Tuesday, August 29, 2017

Mark Zuckerberg amtaka bintiye awe akitoka nje kucheza

Picha ya familia ya Bwana na Bi Zuckerberg

Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook, tajiri Mark Zuckerberg, amemsihi bintiye mdogo kuwa akitoka nje kucheza nje na kufurahia maajabu ya kuwa mtoto, katika barua yenye hisia iliyochapishwa katika ukurasa wake katika mtandao wake wa Facebook.

Barua hiyo ilichapishwa siku ya Jumatatu alipotangaza kuzaliwa kwa mwanawe wa pili aitwaye August, na mkewe Priscilla Chan.

Katika barua ya kina waliyoiandika, wazazi hao wawili walizungumzia kuhusu maajabu ya kuwa mtoto na umuhimu wa kucheza.
Wawili hao waliweka mtandaoni barua kama hiyo kwa binti yao Max mnamo mwaka 2015.
Katika ujumbe hao ambao ameuambatanisha na picha ya familia, Bw Zuckerberg, pia amemhimiza mgeni huyo mchanga "asiwe mkubwa kwa haraka".
"Dunia inaweza kuwa eneo la ushindani mkali. Hiyo ndiyo maana ni muhimu kutafuta nafasi na kwenda nje ili kucheza," ilisema barua hiyo, iliyotiwa saini "Mom and Dad", yaani ''Baba na Mama ''

Wito wa mtoto kwenda kujitambua nje ya nyumba unaonekana kwenda kinyume na lengo kuu la mtandao wa bilionea huyo anayemiliki kampuni kubwa ya mtandao wa kijamii duniani ambaye mara kwa mara hutoa wito wa watu kutumia zaidi mitandao ya kijamii kufahamiana na kujumuika pamoja.

"Matumaini yangu ni kwamba ukimbie mara nyingi sana na kuzunguka sebuleni na pia huko nje kadiri utakavyotaka. Na kisha, natumai kwamba utalala sana," wazazi hao wawili waliandika.
"Utotoni ni hatua nzuri sana. Huwa wawa mtoto mara moja tu, kwa hivyo usitumie muda mwingi sana kufikiria sana kuhusu mustakabali wako."

Trunk Cable Planning & Installation Guide

A trunk can also consist of a cluster of broadcast frequencies, as in a trunked radio system that enables the sharing of a few radio frequency channels among a large group of users.

In telephony, trunks interconnect switching nodes, such as private branch exchanges (PBX) and central offices. In enterprise telephony, the transition from traditional time-division multiplexing (TDM) trunks to SIP trunks began around 2009 to use Voice over IP (VoIP) to connect a PBX to the internet.

Data networks use two types of trunks. First, trunks can carry data from multiple local area networks (LANs) or virtual LANs (VLANs) across a single interconnect between switches or routers, called a trunk port. Second, trunks can bond or aggregate multiple physical links to create a single, higher-capacity, more reliable logical link, which is called port trunking.

A trunk port marks frames with special identifying tags -- defined by IEEE standard 802.1Q for VLAN tags for Ethernet frames -- as they pass between switches, so each frame can be routed to its intended VLAN at the other end of the trunked link. Using port trunking to aggregate links is defined by IEEE standard 802.1aq and by the 802.1AX standard for LANs and metropolitan area networks, as well by various vendor-proprietary methods

Mtu anayefunza kompyuta kutambua harufu

 Raia wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazotumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini Tanzania.
Raia wa Nigeria Oshi Agabi amezindua kompyuta zinazotumia neva za panya katika kongamano la kiteknolojia la TEDGlobal linaloendelea nchini Tanzania.
Mfumo huo umefunzwa kutambua harufu ya vilipuzi na unaweza kutumiwa katika kuimarisha usalama katika viwanja vya ndege, alisema.
Vilevile kifaa hicho kilicho na ukubwa wa modem na kupewa jina Koniku Kore kinaweza kuwa ubongo wa roboti za siku za usoni.
Kampuni kubwa za kiteknolojia, ikiwemo Google hadi Micrososft ziko katika harakati ya kutengeza roboti inayoweza kuwa na akili ya mwanadamu.
Huku kompyuta zikiwa bora kushinda mwanadamu katika kutatua hesabu ngumu, kuna majukumu mengi ambayo yanaweza kufanywa na ubongo wa mwanadamu ikiwemo kuifunza kompyuta kutambua harufu.
Bwana Agabi analenga kubadili baiolojia ya uhandisi ambayo tayari imetimiza uvumbuzi huo.''Biolojia ni Teknolojia''.
Kazi yetu kuu ni kujaribu kuiga ubongo.
Alizindua kifaa hicho cha koniku yapata mwaka mmoja uliopita na amefanikiwa kuchangisha dola milioni moja kama ufadhili na anasema kuwa kifaa hicho kimempatia dola milioni 10 katika mikataba na kampuni za usalama.
Koniku Kore ni kifaa kilichotengezwa kwa kutumia neva na silicon ambacho kina sensa zinazoweza kutambua harufu.
''Unaweza kuzipa neva hizo maelezo ya ni nini unachotaka zifanye ambapo upande wetu tunaziambia kutoa seli zinazoweza kutambua harufu'',alisema